Baada ya mikiki mikiki ya mwaka wa masomo wa 2019/2020, saa ya kufurahi pamoja kwa wanazuoni wote (wastaafu, wahadhiri, wachundo na watawala kwa ujumla wao) imewadia. Ni tarehe 16.12.2020 katika viwanja vya SUA, Campus ya EDWARD MORINGE.
Kwa uchache, SUA CONVOCATION ni jumuiko kuu la Alumni wote wa SUA ambalo hufanyika mara moja kwa mwaka, wiki moja kabla ya kutunuku shahada kwa wahitimu wa shahada za awali hadi uzamivu, maarufu kwa jina la “HOMECOMING WEEK” . Ni Jumuiko na sehemu pekee muhimu inayowakutanisha wanazuoni, wafanyakazi na wahitimu wa SUA mwanzoni mwa mwaka wa masomo wakishiriki michezo mbalimbali na kufurahi pamoja. HOMECOMING WEEK ya mwaka huu inakuja kivingine katika kuileta jamii ya SUA pamoja na yenye furaha kuu.
HOMECOMING WEEK inawaletea TAMASHA la funga mwaka na la msimu litakalo ambatana na michezo mbalimbali tangu asubuhi mpaka jioni. Fikra za safari kwa siku hiyo, labda kama gharama yake haitazibika katika maisha yako yote, weka pembeni. Njoo viwanja vya EDWARD MORINGE, SUA, hutajutia milele yotee!!!!!